Ukiyazingatia haya ndoa yako itakuwa na mafanikio daima
Watu wengi wamekuwa wakifundishwa na kuelewa kwamba tunachotakiwa kuwa nacho ili tuishi kwenye ndoa ni upendo peke yake, upendo ukiwepo basi hakuna haja ya kingine chochote, mengine yatajijia yenyewe tu.
Hiyo imekuwa ni nadharia potofu na wengi kwakushindwa kuelewa wamepata shida sana kwenye ndoa zao. Hapa ninakupa nguzo nyingine muhimu zinazosaidiana na upendo “love” katika kuidumisha ndoa au mapenzi yoyote.
Yafuatayo ndio mambo yanayoweza kuleta mafanikio katika ndoa. UFAHAMU- Kwa kuwa na ufahamu mkubwa.
Ndoa inaweza ikajengwa kwa kufahamu sababu ya ninyi kuwa pamoja, ufahamu wa mambo yapi myazingatie kwenye ndoa yenu, nini mfanye na nini msifanye, yapi mambo hatari na yapi sio hatari. Je unamfahamu mwenzako kwa kiasi gani na je unafahamu nini utegemee kwa jinsia aliyonayo? UELEWA– Ni busara kuelewa mambo ya mahusiano kabla ya kufunga ndoa. Unapaswa kuelewa tabia ya rafiki yako, nguvu na udhaifu wake.
Kuna vitu kwenye ndoa havihitaji majibizano yasiyo lazima, vinahitaji tu uelewa, ukiwa muelewa utapunguza misuguano isiyolazima, elewa haraka kile wmenzako anachotamani umuelewe, penye kuhitaji swali basi uliza ueleweshwe.
Usijifanyishe umeelewa wakati haujaelewa. HEKIMA– Hekima ni muhimu kwenye ndoa. Hii inakuwezesha katika kuamua vizuri kwa ustawi wa ndoa yako.
Ni hekima ndio inakusaidia kufanya maamuzi yasiyo na majuto. Maamuzi ambayo yatazingatia ufahamu wako na uelewa wako.
MAPENZI/UPENDO “Love – Mapenzi yanapaswa kuwa jambo la nne la ndoa yenye mafanikio na sio la kwanza. Unapokuwa na uelewa, ufahamu na hekima basi upendo unakuja kuketi au kutuama sehemu salama kabisa.
Ukiwa na upendo na hivyo vingine havipo basi utashangaa misuguano haiishi. Msisitizo: Ni vizuri ukajiuliza kabla ya kufunga ndoa “Ni kwa nini ninafunga ndoa?”“Nisababu zipi zinanifanya niingie kwenye ndoa?” usipojiuliza swali hili mapema na kulipatia majibu ya kiufasaha basi mbeleni baada ya kuoa au kuolewa unaweza kuja kujiuliza “Ni kwa nini nilifunga ndoa?” “Hivi kwanini nilioa au niliolewa?”.
Bahati mbaya sana wakati unajiuliza maswali haya utakuwa umechelewa “it will be too late”. Ili kuwa na ndoa yenye mafanikio unahitaji ngazi tatu za mahusiano:- Ngazi ya kwanza ya mahusiano ni MUNGU/MUUMBA Hii ndio ngazi ya kwanza ya uhusianona yemye umuhimu mkubwa sana, ngazi hii itaamua kiasi kikubwa cha uhusiano wako na wengine (wa karibu yako na wasio wa karibu yako). Kumshirikisha Mungu katika kila tamanio la moyo wako.
Zungumza na Mungu ni aina gani ya mume au mke unahitaji. Ni aina gani ya familia unayoitamani. Kuwa mwaminifu kwa Mungu kumwambia kila kitu kuhusu mume wako/ mke wako, mwambie kuhusu unachopendelea kama vile rangi, tabia, ngazi ya elimu na mengine yanayohusiana na hayo. Wengi wetu husahau ngazi hii halafu tunapoingia kwenye ndoa kwa kukurupuka tunajikuta vitu vingi sivyo tulivyowahi kutamani na wala havikuwahi kuwa ndoto yetu hapo ndio kukata tama huja kwa kasi na kiu ya kutoka kwenye hiyo ndoa huanza.
Ndoa nyingi sana zimevunjika kwa staili hii. Tafiti zinasema wanandoa wenye mahusiano binafsi mazuri na Muumba wao huweza kuelewan, kuthaminiana na kuheshimiana kwa urahisi zaidi kuliko wale wasio na uhusiano huu. Msisitizo:“Unaweza kuoa/ kuolewa wakati wowote, lakini huwezi kuoa/ kuolewa na yeyote” Ngazi ya pili ya mahusiano ni FAMILIA Familia ni muhimu sana wakati wa kutafuta mchumba.
Uhusiano wa familia wenye nguvu utakusaidia kufanya maamuzi mazuri. Kwanini maamuzi mazuri ni muhimu? Hii ni kwa sababu, kuna tofauti kati ya maumivu kabla ya ndoa na maumivu ya kwenye ndoa.
Ni bora ukaifahamu familia ya huyo mpenzi wako kwa kina ili kupunguza maumivu ya badaye. Bora uumie sasahivi kwa vile utakavyovigundua kuhusu yeye au familia yako kuliko kuvinyamazia halafu vikakuletea maumivu makubwa kesho ukiwa kwenye ndoa tayari. Hakikisha unaifahamu familia ya rafiki yako, jua mahusiano yake na wazazi wake na ndugu zake.
Chunguza kama wana magonjwa ya kurithi, chunguza kama kunatabia z kifamilia, chunguza wazazi na ndugu wanavyomchukulia yeye, angalia ushirikiano wao katika mambo ya kifamilia, chunguza mambo yahusuyo imani zao pia. Fahamu yeye ni mtoto wa ngapi na wako watoto wangapi na wajinsia gani.
Taarifa hizi zitakusaidia sana huko mbeleni Msisitizo:“Utakayefunga nae ndoa anaweza kuwa na matokeo hasi au chanya katika mahusiano yako na familia yako. Baadhi ya migongano ya kifamilia huisha baada ya mtu kufunga ndoa namigogoro mingine huanza baada ya kufunga ndoa. Kwahiyo kuwa makini sana.” Ngazi ya tatu ya mahusiano ni MARAFIKI Unaweza kuwa na marafiki wa karibu kuliko ndugu lakini marafiki hao wanaweza kukushawishi vizuri au vibaya.
Utakayefunga nae ndoa anaweza kutoka miongoni mwa marafiki zako hivyo marafiki wabaya wanaweza kukusababishia ukapata mwenzi mbaya. Utakayefunga nae ndoa anaweza kubadilisha tabia zako na hata kukufanya uwabadili marafiki zako, marafiki wanaokuzunguka pia wanaweza kukuimarisha kiimani au kukufanya dhaifu zaidi.
Usipinge kile unachokisikia kuhusu mwenzi wako kutoka kwamarafiki zako, yale wanayoyasema yanaweza kukusaidia katika kuboresha mahusiano yenu au katika kumfahamu vema zaidi, usiyapuuze wala kuyapinga. Ili kupata mrejesho mzuri kuhusu mpenzi wako basi hauna budi kuwa namarafiki wazuri.Upo uhusiano mkubwa sana wa marafiki ulionao au wanaokuzunguka na tabia uliyonayo. Marafiki wabaya huharibu tabia njema.
Ngazi ya nne ya mahusiano ni MALENGO Malengo yako ya maisha na ndoto zako lazima ziwe na uhusiano na ndoa unayoitaka au uliyonayo. Usifunge ndoa kwa ajili ya watoto, kwa ajili ya tendo la ndoa au kwa ajili ya kupata mtu utakayekuwa naye karibu “companionship”.
Ikiwa umefunga ndoa kwa miaka mitatu au minne na umebaki palepale kimaisha na kimtazamo basi utakuwa haujajua malengo yako au labda unaishi na usiyestahili kuwa nae kwa sababu Mungu wetu ni Mungu wa kuzidisha na sio kupunguza.
Hauingii kwenye ndoa ukaue maono yako bali ukayaongeze na kuyananyua juu. Ongelea ndoto na malengo ya maisha yako ukiwa na marafiki zako. Katika ngazi ya urafiki au uchumba penda sana kuongelea ndoto zako au maono yako na huyo unayempenda ili kujua kama ndoto zenu ni halisi na je hazina migongano au tofauti kubwa? KWANINI NINAFUNGA NDOA? SABABU MBOVU ZA KUFUNGA NDOA.
Kabla sijamaliza mafundisho haya naona ni vema nikikusaidia kufahamu sababu mbovu za kuingia kwenye ndoa. Nimesema awali kwamba watu wengi wanaingia kwenye ndoa kwasababu binafsi na pasipo kujiuliza maswali flani flani. Mtu akishasikia hisia za kusisimka na kuhisi anampenda kijana au dada flani anahisi basi niko tayari kuishi naye maishani kama mume na mke kumbe hiyo sio sababu yamsingi.
Kutokufahamu sababu hizi kumesababisha sana maumivu na majuto mengi baada ya ndoa nyingi kuvunjika huku mmoja akiwa anampenda mwenzake na mwingine anamwona mwenzake kama shetani, kumbe kamwe hakuwahi kumpenda ila alisukumwa na mazingira fulani kuingia kwenye hiyo ndoa. Sababu zenyewe ni hizi zifuatazo; Kuingia kwenye ndoa ili kutafuta kusaidiwa: Usijaribu kuwa na lengo la kufunga ndoa kwa ajili ya kupata msaada, aidha inaweza kuwa msaada wa kijamii au kifedha.
Tunaoa ili tutimize malengo sio kupokea msaada. Kuingia kwenye ndoa kwasababu ya umri. Hatuoi kwa sababu ya umri, umri sio tiketi ya kufunga ndoa. Unaweza kuhamaki sana kwasababu unaona umri wako umeenda (hususani wanawake) mara ukija kumpata mtu ambaye umeamua kukurupuka naye unakuja kujuta zaidi ya ulivyokuwa pekeyako. Angalia vigezo vya msingi kwa mke au mume na sio umri wake au umri wako.
Kupevuka kiakili na kihisia hakusababishwi na umri. Unaweza ukaolewa na mtu anamiaka 40 lakini bado anawaza na kufikiri kama mtoto. Kuingia kwenye ndoa kwasababu ya upweke. Usifunge ndoa kwa sababu ya upweke. Kunatofauti kati ya upweke na kuwa peke yako“there is a difference between loneliness and to be alone”. Upweke unahusu moyo“emotional” na kuwa peke yako inahusu hali ya nje ya mwili “physical”.
Ndoa haiwezi kutatua matatizo ya upweke hususan endapo kama uliyempata sio sahihi kwako. Unaweza ukaolewa au ukaoa na baada ya hapo ukaendelea kuishi mpweke kama ulishindwa kumpata mtu sahihi. Kuingia kwenye ndoa kwa msukumo wa wazazi au marafiki.
Usioe kwa sababu ya msukumo. Usioe au kuolewa kwasababu wazizi wamekwambia uoe au uolewe au kwasababu marafiki zako wengi nao wameoa au wameolewa.
Kumbuka hiyo ndoa unayoenda kuianzishani yakwako na sio ya wazazi wako au marafiki zako. Kuingia kwenye ndoa ili kutafuta kuwa huru. Usifunge ndoa kwa sababu unahitaji kuwa huru kutoka kwa wazai wako. Yamkini wazazi wako wanakubana sana na unashindwa kuishi kwa uhuru au kufanya yale unayoyataka sasa unahisi ukiolewa utatoka kwa wazazi wako na kuwa huru zaidi.
Wako waliowaza kama wewe wakajikuta wamejiingiza kwenye jela ngumu kuliko waliyokuwa nayo awali. Kuingia kwenye ndoa kwasababu ya mimba au mtoto.
Yawezekana sana mmepata mtoto au umempa mtu mimba au umepewa mimba nab ado hamjaingia kwenye ndoa. Kama hamna upendo wa dhati na kama hamkuwa mnamipando ya kuingia kwenye ndoa nawashauri subirini kwanza.
Ni bora kumlea mtoto hamjaoana mkiwa na amani kuliko kuingia kwenye ndoa wakati penzi penu halikuwa la ndoa bali ni la mpito halafu mkashindwa hata kupata muda wa malezi kwa jinsi ambavyo kila siku ni vita moja kwenda vita nyingine.
Wanawake niwasihi sana, tabia za kumtegeshea mwanaume mimba ili akuoe ni ufunguo wa kilio kwa watu wengi sana. Mimba au mtoto sio tuketi ya kuingia kwenye ndoa.

No comments: