Unachotakiwa kufanya ikitokea Condom imepasuka wakati wa tendo
Karibu uhondo TV sehemu pekee utapata habari za siasa,
michezo, burudani na stlye za maisha.
Moja ya kitu leo tunakileta kwako ni hatua nne utakazotakiwa
kufuata endapo kondomu itapasuka wakati wa tendo la ndoa.
Hatua ya kwanza unatakiwa Kuwa mtulivu na baadaye tafuta
kondomu hiyo iliopasuka. Mara nyengine vipande vya mpira huo wa kondomu unaweza
kuingia ndani ya mwili. ingiza vidole vyako ndani yake ishike na kuitoa nje.
Mipira ama vipande vya kondomu vinavyosalia ndani ya mwili
wa binadamu vinaweza kusababisha hasira hivyo basi ni muhimu kuangalia na
kuhakikisha kuwa umetoa kondomu yote.
Hatua ya pili unaambiwa Tumia dawa za kuzuia kushika mimba
iwapo hamjakubaliana kupata mtoto pamoja, Dawa hizi zinapaswa kutumiwa katika
kipindi cha saa 72. Zinauzwa dukani-ikimaanisha kwamba zinapatikana katika
maduka ya dawa. Iwapo huna mpango mbadala unaweza kutumia dawa za kupanga
uzazi.
Hatua ya tatu una shauriwa Kupimwa magonjwa ya zinaa hususan
HIV iwapo hujui hali ya mwenzako Nenda katika kituo cha dharura karibu nawe na
umwambie daktari yaliofanyika.
Aidha unaweza kuchukua dawa aina ya Post Exposure
Prophylaxis (PEP) katika kipindi cha saa 72.
PEP ni mchanganyiko wa dawa za kukabiliana dhidi ya virusi
vya ukimwi ambazo zinakuzuiwa kutoambukizwa HIV iwapo mwenzako ni mwathiriwa.
Kumbuka kwamba kila ugonjwa wa zinaa una muda wake wakati
unapoambukizwa na wakati utakapoonyesha unapopimwa. Unashauriwa kufanyiwa
vipimo zaidi vya vya magonjwa ya zinaa baada ya mwezi na baada ya miezi sita
ili kujua hali yako.
Hatua nyingine unayoshauriwa ni kuChunguza kilichotokea
Wapenzi wengi huruka hatua hii-hayo ni makosa makubwa, kwa
sababu ni hadi utakapoelewa ni kwa nini mpira huo ulipasuka ndiposa unaweza
kujiweka katika hatari nyengine. Hivyobasi jiulize swali hilo.
Je mpira huo wa kondomu ulipasuka kwa sababu wakati wake
ulikuwa umekwisha?
Iwapo hilo ni kweli unaweza kutupa paketi ulio nayo na
kununua pakiti nyengine . Ziweke mbali na joto ama hata mwangaza na usizibebe
katika kipochi chako na usizifungue kwa kutumia makasi ama meno.
-Je mpira huo wa kondomu ulipasuka kwa sababu ulivaliwa
vibaya?
Weka mafuta ndani ya kondomu hiyo iwapo utahitaji , lakini
hakikisha kuwa hutumii mafuta nje ya mpira huo, Finya eneo la mbele la mpira
huo ili kutoa upepo Ukishavaa kondomu hiyo wacha nafasi mbele ya mpira huo
ambayo itaweka shahawa.
-Je mpira huo wa kondomu ulipasuka kwa kuwa ulikuwa mdogo
sana?
Pima ukubwa wa uume wake wakati unaposimama. Halafu uangalie
chapisho hili ili kujua ni ukubwa gani wa kondomu unaopaswa kutumia. Unaweza
kushangaa!
-Je mnpira huo wa kondomu ulipasuka baada ya kuupaka mafuta?
Utumizi wa mafuta kama vile ya Olive ama mafuta ya nazi
unaweza kuwa hatari kwasababu yanaweza kufanya kondomu kupasuka
Kumbuka kwamba ajali za kondomu zinaweza kumtokea mtu
yeyote.
Basi kwa habari za siasasa , michezo, burudani na style za
maisha subscribe youtube channel yetu ili uzipate kwa haraka kila tutakapokuwa
tunaweka
No comments: