ALIYESIMAMISHWA NA MWIGULU ARUDI KAZINI
Miongoni mwa habari kubwa mitandaoni ni pamoja na Picha
inayosambaa ikimuonesha Mkurugenzi wa Idara ya Usajili wa Vyama vya Kijamii
katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi Marlin Komba ambaye alisimamishwa kazi
Juni 8, 2018 na Aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo Mwigulu Nchemba kutokana na
barua iliyosambaa mtandaoni ikiwa na sahihi yake. Barua hiyo ililitaka kanisa
la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) kufuta waraka wake Pasaka.
Picha hii inayomuonesha Marlin Komba akisalimiana na Waziri mpya wa Wizara
hiyo Kangi Lugola imetoa tafsiri kwa watu wengi kwamba Marlin Komba amerudi
kazini .
Kwa mastori makali kama haya endelea kukaa karibu na chaneli yetu ya
UHONDO TV pamoja na Uhondo Habari kwenye mitandao ya kijamii.
No comments: