Header Ads

Alichokifanya Rais Magufuli baada ya Waziri Kigwangalla kupata ajali

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli jioni ya tarehe 04 Agosti, 2018 ameungana na viongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, kumpokea Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangala ambaye amesafirishwa kwa ndege kutoka Arusha alikopata ajali leo asubuhi, kuja Jijini Dar es Salaam kwa matibabu zaidi.


Dkt. Kigwangalla aliyekuwa akisafiri kutoka Arusha kwenda Dodoma amepata ajali leo majira ya saa 12:15 asubuhi katikati ya vijiji vya Mdolii na Minjingu Wilaya ya Babati Mkoani Manyara baada ya gari lake kupinduka na kusababisha kifo cha Afisa Habari wa Wizara ya Maliasili na Utalii Bw. Hamza Temba na wengine watano akiwemo Dkt. Kigwangalla kuumia.


Baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, Dkt. Kigwangalla amepelekwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu.



Kwa mastori makali kama haya usiache ku-Subscribe YOUTUBE yetu ya Uhondo TV lakini pia Download App yetu ya Uhondo Habari ili uwe wa kwanza kila tunapoweka habari mpya kila wakati.

No comments:

Powered by Blogger.