Header Ads

Maajabu ya mtu aliyetolewa betri na redio ndani ya tumbo

Inawezekana hili likawa ni moja ya tukio la ajabu kutokea ambapo kijana mmoja kutokea mkoani Kagera afanyiwa upasuaji wa tumbo na kukutwa na vitu mbalimbali ikiwemo kijiko, betri ndogo ya redio na vitu vingine kadhaa.

Kijana huyo ambaye ni mgonjwa wa akili alifanyiwa upasuaji huo katika hospitali teule ya Missenye, Mugana na kukutwa pia na viberiti vya gesi, mfuko, vitambaa na ganda la limao. Dkt. Eliud Nyonyi aliyeshiriki kumfanyia upasuaji mgonjwa huyo, Eliud Novart (25) amesema baada ya vitu hivyo kutolewa hali ya mgonjwa huyo inaendelea vizuri.

Mganga Mkuu wa Missenye, Dkt. Hamis Abdallah alisema mgonjwa alifikishwa katika Hospitali ya Mugana baada ya kupatiwa rufaa na Hospitali ya Nyakahanga, wilayani Karagwe. Vituko vingine tena leo kwenye mnada makondana ya Makonda

No comments:

Powered by Blogger.