Header Ads

Aliyezaa na Casto ajibu mapigo “Tunda hana lolote, Casto ni mchafu”



Kufuatia 'Couple' mpya inayotikisa jiji kwa sasa ya mtangazaji wa Clouds, Casto Dickson na Video queen, Tunda, mwanamke mmoja ambaye ni mzazi mwenza wa mtangazaji huyo anayefahamika kwa jina la Don Posh, ameibuka na kuweka bayana kuwa wawili hao hawawezi kuwa na uhusiano kamwe ila ni kiki tu.

Posh amesema kuwa bado anampenda mzazi mwenziye huyo, na kusema kuwa hakuna mwanamke atakayetokea kupendwa na Casto kama yeye kwani alichompatia hawezi kupatiwa na mwanamke mwingine yeyote.

Posh ameongeza kuwa Casto ni mlevi sana, na kuwa hapendi vile ambavyo Casto anashikana shikana na Tunda na kuachia video zao mitandaoni, huku akichanganya maelezo yake baada ya kusema pia kuwa hampendi tena kutokana na uchafu wake wa kutembea na wanawake hovyo hadi mahausigeli. 



Sasa unaweza kuzipata habari zote kubwa Duniani kwa haraka ndani ya saa 24 kupitia Application ya UHONDO HABARI kwa kubofya hapa>>> http://bit.ly/2tQOFYW 
http://bit.ly/2tQOFYW

No comments:

Powered by Blogger.