Header Ads

Alichokijibu Neymar baada ya tuhuma za kujiangusha uwanjani



Mshambuliaji wa Brazil, Neymar amejitokeza na kujetetea juu ya kitendo chake cha kuonekana kama amejigaragaza mno wakati alipochezewa faulo na Miguel Layun ukilinganisha na namna hata tukio hilo lilivtokea, hayo yamekuja baada ya kupata lawama nyingi kutoka kwa wapenzi wa soka na baadhi ya mitandao ya kijamii.

Neymar mwenye umri wa miaka 26 amejitupatupa mno alipochezewa faulo na mchezaji wa timu ya taifa ya Mexico, Miguel Layun mchezo wa 16 bora wa kuwania kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya kombe la dunia na kumalizika kwa matokeo ya Brizil kupata shindi wa mabao 2 – 0.

Mchezaji huyo ghali zaidi duniani anayekipiga kwenye klabu ya Paris St-Germain amesema kuwa alikuwa akijiskia maumivu makali.


Sasa unaweza kuzipata habari zote kubwa Duniani kwa haraka kupitia Application ya UHONDO HABARI kwa kubofya hapa>>> http://bit.ly/2tQOFYW



No comments:

Powered by Blogger.