NOMA SANA: Raia wa kigeni akitaka kuoa analipa kodi
Miongoni mwa mastori makali ya kukusogezea leo ni pamoja na
hii ya kutoa kwa Mfalme Mswati wa swaziland ametuma mswaada bungeni akitaka
kutungwa kwa sheria mpya kwa raia kutoka nje ya nchi hiyo kulipa kodi
watakapofunga ndoa na wanawake nchini Swaziland kwa kutozwa kiasi cha dola 2,200.
Unaambiwa
kwamba Mfalme Mswati ametuma mswaada huo bungeni huku akidai kuwa sheria
hiyo ni kwa ajili ya kuwalinda wanawake nchini humo.
“ Lengo la sheria hii ni kuwalinda wanawake na
matendo ya unyanyasaji kutoka kwa wapenzi wao wa kigeni wanaotumia njia ya kuoa
wanawake wetu kwa ajili ya kupata uraia” hayo yamenukuliwa kutoka kwa Msemaji wa
Serikali Percy Simelane.
Aidha mswada huo umepingwa vikali na mmoja wa wanaharakati
wa kutetea haki za wanawake Dumsane Dlamini akidai kuwa sheria hiyo itawanyima
haki wanawawake nchini Swaziland maana wanawake hao huwapenda wanaume wa kigeni
kwa utanashati na wanajua thamani ya mapenzi.
Kwa mastori makali kama haya endelea kukaa karibu na Uhondo Habari ndani ya saa 24
No comments: