Mchungaji akamatwa kwa kuuza tiketi za kwenda Mbinguni
Mchungaji mmoja
aliyefahamika kwa jina la
Tito Wats, anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kuwauzia watu
tiketi alizodai ni za kuingilia Mbinguni
Anasema alitokewa na Yesu,
akampa tiketi ili awagawie watu wenye dhambi ili siku ikifika waingilie kwenye
mageti ya mbinguni.
Bei ya tiketi moja ni USD
500 zaidi ya Milioni moja ya Kitanzania.
Alipokamatwa amesema hajali,
maana anajua anateswa kwa sababu ya kufanya kazi ya Mungu.
Watu wengi wanaandamana
kupinga kukamatwa kwa mchungaji wao, kwa sababu hizo pesa wanazotoa ni zao, na
kwa hiyari yao kwa ajili ya uzima wao.
No comments: