Header Ads

Pigo lingine zito kwa Freeman Mbowe

Karibu katika kijiwe cha Uhondo na miongoni mwa mastori ya town leo ni hii ya kutokea Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO) Mkoani Kilimanjaro limeikatia umeme Aish Hotel inayomilikuwa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe baada ya kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya Tsh. Milioni 10 kwa kuiba umeme Meneja wa TANESCO Mkoani humo.

Mahawa Mkaka amesema wamebaini jana Septemba 14 kuwa wamejiunganishia umeme na kuharibu miundombinu yake Alieleza kuwa "Baada ya kupata taarifa kutoka vyanzo vyetu tulienda kwenye hoteli hiyo kufanya ukaguzi, tukabaini wameharibu mita na kujiunganishia umeme kinyemela." 

Aliongeza kuwa "Hasara hiyo ya zaidi ya Tsh. Milioni 10 ni kwa tathmini ya awali na sasa hivi tunasubiri hesabu kutoka TANESCO Makao Makuu."

Kwa mastori makali kama haya usiache Ku-Subscribe YOUTUBE CHANEL yetu ya UHONDO TV lakini pia Download App yetu ya UHONDO HABARI ili uwe wa kwanza kila tunapoweka habari mpya kila wakati.

No comments:

Powered by Blogger.