Header Ads

Daktari aanika madhara ya kukatwa utumbo kama alivyofanya Wema Sepetu


Kwa mujibu wa daktari huyo, njia hiyo ya kupunguza unene ambayo wengi huijua kama kukatwa utumbo kitaalum inaitwa Gastric Band ambapo sehemu ya tumbo la binadamu inabanwa ili kulipunguza ukubwa na kuruhusu kiasi kidogo cha chakula kuingia. “Ni njia ya kitaalam ya kupunguza unene, kinachofanyika ni kupunguza ukubwa wa tumbo kwa kulibana katika sehemu ya juu ili mtu anapokula chakula kidogo tu ajisikie ameshiba. Hali hiyo humfanya kadiri siku zinavyokwenda kupungua unene,” alisema daktari huyo na kuongeza:

Image result for wema sepetu
“Ni njia inayoshauriwa kidaktari ya kupunguza unene lakini mbali na faida hiyo, kuna madhara yanayoweza kuwapata wanaofanya uamuzi huu. “Kwa mfano, lengo lako linaweza kuwa ni kupungua lakini sasa ukakonda kupitiliza, hali ambayo pia kiafya siyo sawa. Lakini pia, tiba hii ya kupunguza unene inafanyika kwa kufanyiwa upasuaji ambapo damu nyingi inaweza kupotea na kusababisha madhara makubwa.

Madhara mengine yanayosababishwa na upasuaji huu, ni mwili kushindwa kuzikubali dawa za usingizi (Anasthetics) ambazo kwa kawaida mgonjwa yeyote anayefanyiwa upasuaji huchomwa kabla ya upasuaji. Hali hii ikitokea, maana yake ni kwamba mgonjwa anaweza kuzinduka wakati upasuaji ukiendelea na kusababisha kifo.

Matatizo mengine yanayoweza kusababishwa na upasuaji huu, ni mwili kupata mzio (allergy), kupata matatizo ya kupumua, damu kuganda kwenye miguu na kwenye mapafu, kuishiwa damu, kupata maambukizi kwenye damu na kupatwa na shambulio la moyo au kiharusi wakati wa upasuaji au baada ya kumalizika kwa upasuaji.

Pia kifaa maalum kinachowekwa tumboni baada ya upasuaji, kinaweza kuhama sehemu kilipowekwa au kikayeyuka na kusababisha madhara kwa mhusika, ambapo atalazimika kufanyiwa tena upasuaji. Utafiti unaonesha kwamba, kati ya asilimia 15- 60 ya watu waliofanyiwa upasuaji huu, hulazimika kufanyiwa upasuaji mwingine ili kurekebisha dosari zilizotokea awali.

Baada ya upasuaji, mhusika anatakiwa kufuata masharti ya vyakula, vinginevyo atatapika sana na kupatwa na tatizo la kutanuka kwa koo.

No comments:

Powered by Blogger.