Header Ads

Huu ndio ujumbe wa Dully Sykes kwa wasanii wote wapya



Msanii wa Bongo Flava, Dully Sykes amesema wasanii wa zamani kuwachukia wasanii wa sasa katika muziki huo haina maana yoyote kwani wao ndio wanafanya muziki huo unazidi kukua.

Muimbaji huyo anayetamba na ngoma yake mpya ‘Zoom’ ameiambia TV E kuwa sababu ya wasanii hao kuwachukia wenzao ni kutokana na kukosa ubunifu. “Nachukia sana wasanii wa zamani wanaoponda wasanii wa kileo, kwa sababu ukileta upendo wa wasanii wa kileo, unaweza kujenga kitu kimoja kikubwa sana. Wengi wanapotea kwa sababu wanachukia wasanii wa kileo,” amesema. “Wasanii wa zamani hawanaga ubunifu, bado wanataka kuwasema wasanii wa kileo. Kiukweli mimi muziki wangu unakua kila siku kwa sababu ya wasanii wa kileo,” amesisitiza Dully.

Ameendelea kwa kusema wasanii wa kileo hawaharibu muziki kwa sababu ndio wanafanya muziki unakuwa mkubwa na endapo wangewaaachia wa zamani wafanye wenyewe Bongo Flava isingefika ilipo sasa.

No comments:

Powered by Blogger.