Mkwanja atakaoingiza Ronaldo akijiunga na Juventus
Juventus wameanza kuonja mafanikio ya kuhusishwa na kumsaini mwanasoka bora wa dunia Cristiano Ronaldo tayari, thamani ya klabu imepanda kwa asilimia 22 ndani ya siku 3 – thamani ya mtaji wa klabu imeongezeka kwa zaidi ya €160m sawa na billioni 425 za kitanzania.
Kwa siku 3 tu tangu taarifa za usajili wake ambao unatajwa kuwagharimu Juventus kiasi cha €100m kumeshaanza kuinufaisha klabu hiyo ya Turin. Ripoti kutoka kwenye soko la hisa – thamani ya klabu ya Juventus imekuwa kwa asilimia 22 – mtajinwa klabu umekuwa kutoka €665m mpaka €825m, kwa mujibu wa Calcio e Finanza. Kwa upande wa Ronaldo, endapo atajiunga na Juventus atakuwa analipwa mshahara pekee €30m sawa na zaidi ya billioni 80 kwa mwaka – kabla ya kupata maslahi mengine.
Makampuni mengine ya familia ya mmiliki wa Juventus bwana Agnelli (Ferrari, FIAT and Jeep) – yatasaidia kwenye ulipaji wa mshahara huo. Cristiano pia anatarajiwa kupewa mkataba mwingine wa kumongezea kipato kwa kufanywa kuwa balozi wa Ferrari duniani.
Mkataba ambao utamuingizia kiasi kingine cha €20m - zaidi ya bilionj 50 za kitanzania kwa mwaka. Kwa maana hiyo tayari Ronaldo kupitia mahusiano yake na Juventus moja kwa moja yatamuingizia kiasi cha €50m kwa mwaka.
No comments: