Ajali nyingine tena yatokea Mbeya na kuua
Watu watano wanadaiwa kufariki dunia usiku wa kuamkia leo katika ajali iliyohusisha lori pamoja na gari dogo aina ya Noah eneo la mteremko wa mlima Igawilo mkoani Mbeya.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo ambao walikuwepo wamesema kwamba huenda chanzo cha ajali hiyo ni lori ambalo lilifeli breki na kuyagonga magari mengine matatu ikiwemo la TANESCO na kampuni ya CocaCola pamoja na hiyo Noah ambayo ilikuwa na abiria watatu ambao wawili inahofiwa wamefariki papo hapo na mmoja amekimbizwa hospitali rufaa ya Mbeya kupatiwa matibabu.
Dereva wa lori na msaidizi wake wanahofiwa kwamba wamefariki dunia papo hapo na juhudi za kuondoa maiti zao zimekua zikiendelea wakati wa kutuma taarifa hii. Ajali hii imekuja masaa machache tu baada ya waziri mpya wa Mambo ya Ndani Mhe. Kangi Lugola kumaliza ziara yake mkoani Mbeya ambapo pamoja na mambo mengine amevunja kamati na mabaraza ya usalama barabarani nchi nzima kwa nia ya kujipanga upya katika kupambana na jang hilo sugu la Taifa.
Kwa mastori makali kama haya usisahau kudownload App yetu ya UHONDO HABARI kupitia PLAY STORE kwenye simu yako na Subscribe UHONDO TV kwenye YOUTUBE
No comments: